Wadau, leo nimepokea habari za kusikitisha za kifo cha Msanii, Adam Kuambiana. Mwenyezi Mungu ailaze roho yake mahala pema mbinguni. Amen.
KUTOKA
LUKWANGULE BLOG
|
The Late Adam Philip Kuambiana |
HABARI
haziko wazi lakini marafiki w akaribu wamethibitisha kwamba dairekta
anayekuja juu, muigizaji na mwandishi wa sinema Adam Phillip Kuambiana
PICHANI amefariki saa chache zilizopita.
Mkali huyo mwenye tabia
'ngumu ' (hana simu ya mkononi) labda sasa, ameshiriki kama muigizaji au
dairekta katika sinema Lukuki na amekufa akikimbizwa hospitali ya Sinza
palestina.
Hizi ni baadhi tu ya kazi zake njema:
Danija
Faith More Fire|
Bad Luck
Scola
The Boss
Mr.Nobody
Radhi ya Mke
Lost Sons
Chaguo Langu
My Fiance
Jesica
Life of Sandra
Basilisa
My Flower
Regina
|
The Late Adam Kuambiana |
Born Again
Its Too Late
Fake Pastors
Nilimpenda sana kuambiana katika filamu ya Fake Pastors.
Vijana
watanashati Vicent Kigosi (Patric) na Adam Philip Kuambiana (Petro)
waliohitumu Chuo Kikuu cha Mzumbe, Morogoro Vichwani mwao wanaelewa kitu
kimoja tu walichoambiwa tangu utotoni kuwa ukiwa na digree masiha
yatakuwa rahisi jambo ambalo baada ya kuingia mitaani wanakuta ni
tofauti kwani hakuna ajira na maisha yanakuwa magumu sana kwao.
Baada
ya kutembea katika ofisi moja hadi nyingine wakitafuta kazi bila
mafanikio, hatimaye wanagundua kuanzisha kanisa ndio suluhisho pekee
walilobakiza hivyo wanaamua kuwa wachungaji wa uongo (Fake Pastors) na
kuanzisha kanisa kwa lengo la kujitajirisha badala ya kumtumikia Mungu,
kazi yao inakuwa ni kuwakamua waumini fedha na mali walizonazo.
Kwakufanya
hivyo wanajikusanyia utajiri mkubwa hasa baada ya misaada kuanzia
kuingia kutoka nje kwa wahisani, baadala ya kufanya kazi ya Mungu wao
wanazitumia fedha hizo katika anasa wakilewa pombe na kununua Malaya
usiku na ifikapo asubuhi wanahubiri injili kama kawaida na kuwafanya
waamini wazidi kuwakubali. Baadae walijingiza katika biashara haramu
dawa za kulevya ndipo Mungu Mbinguni alipoamua kuingilia kati na
kuwaadhibu vibaya.
Cast: Adam Philip Huambiana (Petro), Vicent Kigosi (Ray), Jokette Mwegelo (Jach), Lisa Jensen (Lisa), Blandina Chagula
Producer- Vicent Kigosi, Executive Producer- Eric Shigongo, Director- Gervas Kasiga