Showing posts with label Mbunge. Show all posts
Showing posts with label Mbunge. Show all posts
Wednesday, March 01, 2017
Saturday, February 07, 2015
Mbunge na Walinzi wake Wauawa Kenya!
The Late MP for Kabete, George Muchai |
NAIROBI, Kenya (AP) - Kenyan police say a lawmaker has been shot and killed on a street in the capital, Nairobi, by masked gunmen.
Nairobi Central Police Chief Paul Wanjama said the lawmaker, George Muchai, was killed alongside his two bodyguards and a driver after they stopped to buy a newspaper from a vendor early Saturday. He said the gunmen then sped away in their car.
The killings are likely to stoke insecurity fears in Kenya, which has also been dealing with occasional terrorist attacks mounted by Islamic militants seeking revenge over Kenyan military involvement in Somalia.
Former Prime Minister Raila Odinga said in a statement that Kenya "is bleeding and an atmosphere of fear and hopelessness is spreading" across the country.
Murder Scene |
Saturday, January 10, 2015
Mr Sugu Apata Ajalia ya Gari Iringa
Kutoka Facebook:
Picha zikionesha Mbunge wa Mbeya mjini Mr Sugu na rafiki yake wakiwa kando ya gari lao baada ya kupinduka katika mteremko wa Kitongo leo.
MBUNGE wa jimbo la Mbeya mjini Joseph Mbilinyi a.k.a Mr Sugu (Chadema) amenusurika kifo baada ya gari lake kupinduka katika mlima wa Kitonga wilaya ya Kilolo kwenye barabara kuu ya Iringa - Dar es Salaam.
Ajali hiyo imetokea mchana wa leo wakati gari la mbunge huyo likiwa na watu wengine wanne likitokea Mbeya kuelekea jijini Dar es Salaam.

Hata hivyo vyanzo vya habari hizi viliueleza mtandao huu wa www.matukiodaima.co.tz kuwa mbunge huyo amepatwa na michubuko kiasi na hakuna aliyepoteza maisha katika ajali hiyo .
Kamanda wa polisi wa mkoa wa Iringa Ramadhan Mungi akimethibitisha kutokea kwa ajali hiyo japo amesema taarifa kamili zitapatikana mara baada ya askari waliokwenda eneo la tukio kurejea.
Kamanda wa polisi wa mkoa wa Iringa Ramadhan Mungi akimethibitisha kutokea kwa ajali hiyo japo amesema taarifa kamili zitapatikana mara baada ya askari waliokwenda eneo la tukio kurejea.
Saturday, December 20, 2014
Mbunge Ishungisa Afariki na Mjukuu Wake
MBUNGE ISHUNGISA AFARIKI NA MJUKUU WAKE
Na Happiness Katabazi
ALIYEKUWA Mbunge wa Pili , wa Jimbo la Karagwe ambaye alifariki Jana jioni, Laurent Ishungisa , mjukuu wake ambaye ni Mfanyakazi wa Kampuni ya Simu ya TIGO, Gody Tibyampasha naye amefariki alfajiri ya kuamkia Leo Katika eneo la Skansaka karibu na Mitambo ya IPTL Wilaya ya Kinondoni kwa ajali ya Gari.
Kwa mujibu wa Msemaji wa msiba wa Inshungisa, Medard Birusya alisema Gody alikutwa na umauti huo wakati akiendesha gari lake wakati akitokea kwenye msiba wa Babu yake Mabibo Hosteli kurudi nyumbani wake Tegeta kupumzika.Miili ya marehemu wote imeifadhiwa Katika Hospitali ya Mwananyamala.
Birusya akitangaza Ratiba ya misiba hiyo miwili jinsi watakavyoiendesha hivi punde nyumbani kwa Mtoto wa marehemu Ishungisa, Grace Byampanju eneo la Mabibo Hosteli, alisema msiba wa mbunge Ishungisa uliokuwa ukifanyika Mabibo Hosteli kuanzia Kesho asubuhi utaamishiwa nyumbani kwa wazazi wa marehemu Gody eneo la Tegeta kwasababu Mama Mzazi wa Gody ni Mtoto pia wa marehemu Ishungisa.Baba wa Gody ni Daktari Mstaafu Dk. Dominic Tibyampasha.
Birusya alisema , Jumatatu miili ya marehemu ambao ni Babu na Mjukuu wake itaagwa Tegeta na Kisha itasafirishwa kupelekwa Wilayani Karagwe kwa ajili ya kuzikwa.
Birusya alisema Mbunge Ishungisa atazikwa Disemba 24 Mwaka huu ,Katika Kijiji Cha Nyakaiga na mjukuu wake marehemu Gody ambaye ameacha Mke na Mtoto wa Miezi mitatu atazikwa Disemba 25 Mwaka huu Katika Kijiji Cha Kiruruma. Ni masikitiko makubwa.Mungu tunaomba utupe moyo wa subira na uvumilivu maana huyu Israel Mtoa roho za watu anafanyakazi yake bila huruma.
Ishungisa alifariki Disemba 19 mwaka huu, nyumbani kwa mwanae Grace, Mabibo Hosteli baada ya kuugua kwa muda mrefu.Miili ya marehemu wote imeifadhiwa Katika Hospitali ya Mwananyamala Dar Es Salaam.
Chanzo: Facebook: Happy Katabazi
Disemba 20 Mwaka 2014.

Labels:
Ajali. Car Accident,
Ishungisa,
Karagwe,
Mbunge,
Msiba
Saturday, October 25, 2014
Mh. Shy-Rose Bhanji Ajibu Shutuma Dhidi Yake
Mh. Shy-Rose Bhanji |
Mimi
Shy-Rose Bhanji, Mbunge wa Afrika Mashariki-Tanzania, ninapinga vikali
na kwa nguvu zote shutuma zilizotolewa dhidi yangu kupitia mitandao
mbalimbali ya kijamii.
Shutuma hizi hazina ukweli wowote na
zinalenga, si kuniharibia, bali kuchafua sifa yangu na utendaji kazi
wangu katika Bunge la Afrika Mashariki.
Lengo kuu la shutuma hizo
ni kunivunja nguvu na ari ya kutetea maslahi ya nchi yangu na
Watanzania wenzangu kwani daima nimekuwa kikwazo na mwiba kwenye ajenda
zinazokiuka maslahi ya Tanzania.
Kwa mfano ardhi ya Tanzania
kugawiwa kwa wana Jumuiya ya Afrika Mashariki ni kinyume na Sera ya
Tanzania. Nimekuwa miongoni mwa wabunge wa Tanzania tulio mbele katika
kulipinga suala hilo. Sishangai likinijengea uadui.
Isitoshe,
kwenye ajenda ya kumuondoa madarakani Spika wa EALA, Dk. Margaret Zziwa,
nilisimama kidete kwa kutounga mkono kwa sababu halikuwa na maslahi ya
Tanzania na yalikuwa kinyume na malengo ya ushirikiano wa Jumuiya nzima.
Hoja ya kumuondoa Spika ilikuwa ni sehemu ya ‘mchezo mchafu’ ya ajenda
ya siri ya kumweka kwenye nafasi hiyo mjumbe mwingine kwa maslahi ya
wachache.
Jaribio hili la kumuondoka Spika lilifanywa na
kushindikana mara tatu baada ya kukosa sahihi za kutosha kutoka
Tanzania, ikiwamo ya kwangu.
Baada ya kampeni ya kumwondoa Spika
kushindwa, wabunge kadhaa walikuwa wanasusia vikao vya Bunge wakati
wameshachukua posho za vikao. Kwa mfano kikao kilichofanyika hivi
karibuni hapa Dar es Salaam.
Malumbano ndio yamekuwa yakitawala
na kuinyima Bunge akidi ya kuendelea na ajenda za mtangamano. Huu ni
usaliti wa wazi kwa nchi zilizowachagua na kuwatuma katika Bunge la
EALA.
Ukijaribu kuwaasa kwamba mwenendo huo si sahihi, unageuka kuwa adui.
Na sasa wameamua kunitukana na kuzusha tuhuma kadhaa kupitia mitandao
ya kijamii ambako yote ni utunzi wa kisanii usiokuwa na chembe ya
ukweli, uhalali wala ushahidi.
Wahenga walisema ‘akutukanaye hakuchagulii tusi’. Walete ushahidi wa tuhuma zote dhidi yangu.
Kwa mfano, shutuma kwamba nililewa pombe ndani ya ndege, kuvunja chupa,
kufanya fujo na kufungwa pingu wakati wa safari ya Ubelgiji si kweli
hata kidogo.
Kama hizi tuhuma ni za kweli, kwanini hazikupelekwa polisi, serikalini au vyombo vingine vya sheria baada tu ya tukio?
Ijewe wamesubiri wiki mbili baada ya madai hayo ya tukio la kutunga
ndipo wajitokeze wakati wa kikao kinachoendelea mjini Kigali, Rwanda?
Kwanini wasubiri kikao cha Kigali ndipo uzushi huu utolewe?
Tuhuma kwamba nimewatukana marais wa nchi tatu hazina mashiko isipokuwa
kuhalalisha kampeni ya wale wanaonichafua na kuibua chuki kwa maraisi na
raia katika nchi za Kenya, Rwanda na Burundi.
Ninayo heshima
kubwa sana kwa marais wa nchi zote tano na raia wa nchi wanachama ambako
mara zote nimepokewa na kuishi kwa amani na upendo katika nchi hizo.
Naahidi kuedeleza heshima hii.
Hainiingii kichwani ni wapi
nilipoteza heshima hii isipokuwa kwa wale wasionitakia mema ambao
wamekusudia kufanikisha ajenda zao.
Shutuma zote dhidi yangu zimetengenezwa na watu ambao hatushabihiani katika hoja zetu na sishangai kwa hilo.
Mimi ni Mtanzania na ni Mbunge wa Tanzania. Hivyo nina wajibu wa
kulinda na kutetea maslahi ya Watanzania ili kuleta mtangamano wenye
uwiano sawa kwa nchi zote wanachama.
Ninaahidi nitaendelea
kuwatumikia Watanzania kwa nguvu zangu zote na kutoa ushirikiano kwa
wabunge wengine wa EALA kwa manufaa ya Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Nimeyasema haya nikiamini kuwa: “Uongo ukiachwa usemwe mara nyingi unaweza kuaminiwa kuwa ni ukweli.”
Umoja Wetu Ni Nguzo Yetu
Mungu ibariki Afrika Mashariki
Asanteni,
Shy-Rose Bhanji
Mbunge EALA
Shy-Rose Bhanji
Mbunge EALA
Monday, July 07, 2014
Saturday, March 01, 2014
Rasimu ya Katiba imewashau Vijana! - Makonda
Mimi ni Kijana, ninayoyazungumza,ninayoyafanya yana reflect
uhalisia huo. Hivyo kwa wito wa Ujana najikuta nashawishika sana kuongeza
umakini katika masuala yahusuyo vijana hasa kwenye Katiba.
Ni ajabu lakini kweli kuwa sehemu inayotaja juu ya Haki na Wajibu wa Vijana katika Rasimu yote ni Ibara ya 44 tu, tena inataja kwa ujumla wake bila hata kuweka ibara ndogo ama vipengele vya ufafanuzi.
Ibara hiyo inasema;

"..kila kijana ana haki na wajibu wa kushiriki kikamilifu katika shughuli za maendeleo ya Jamhuri ya Muungano pamoja na jamii kwa ujumla, na kwa mantiki hiyo, Serikali ya Jamhuri ya Muungano, serikali za nchi washirika na jamii zitahakikisha kuwa vijana wanawekewa mazingira mazuri ya kuwa "Raia Wema" na kupatiwa fursa za kushiriki kikamilifu katika nyanja za kisiasa, kiuchumi, kijamii na kiutamaduni..."
Sikuwa nategemea huu unaweza ukawa ndio mwisho wa maelezo ya Rasimu kuhusu Vijana. Nilitegemea nitakuta vipengele vinavyobainisha namna vijana watakavyonufaika na rasilimali, namna ambavyo sheria ndogo na taratibu baguzi ktk upatikanaji wa ajira na fursa zitakavyobainishwa kikatiba ili kumaliza kabisa matatizo ya Vijana.
Nilidhani Rasimu itaweka bayana Uanzishwaji wa Baraza La Vijana la Taifa ili kiwe chombo cha kikatiba cha Vijana.
Nikitumia fursa na nafasi yangu kama mbunge wa bunge maalum la Katiba zipo hoja hizo kuu (3) tatu ambazo nitazisimamia ziingie kwenye Katiba kwa manufaa na mustakabal mwema wa Vijana bila kujali tofauti ya itikadi, dini ama kabila.
Na nakaribisha mawazo na michango ya fikra ktk hoja zihusuzo Vijana.
IMETOLEWA NA:
PAUL MAKONDA.
MBUNGE WA BUNGE MAALUM LA KATIBA.
Thursday, March 28, 2013
Mazishi ya Mh. Khamis Yatakuwa Kesho Mjini Pemba
The Late Honourable Salim Hemed Khamis (MP Chambani Pemba -CUF) |
MAZISHI ya aliyekuwa Mbunge wa CUF, Jimbo la Chambani Pemba kisiwani Zanzibar, Marehemu, Salim Hemed Khamis, (62), yanataraji kufanyika kesho (Ijumaa Machi 29, 2013) mchana mjini Pemba.
Tarifa za awali kutoka Chama cha Wananchi CUF, zinasema kuwa Mwili wa Marehemu, Khamis utaagwa kesho asubuhi kuanzia majira ya saa 2:30-4:00 katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam ambapo Viongozi mbalimbali wa kitaifa na Kimataifa pamoja na wananchi na Wanachama wa CUF watapata fursa ya kutoa heshima za mwisho kwa Marehemu.
Taarifa hiyo ya Naibu Katibu Mkuu wa CUF, Julis Mtatiro inasema kuwa Msafara utaondoka Karimjee saa 4:00 kuelekea uwaja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere ambapo Msafara wa Ndege 2 utaondoka kwenda Pemba.
Saa saba mchana mazishi yatafanyika huko Pemba na maazishi hayo yataongozwa na Viongozi wa serikali, Wabunge na CUF.
Mtatiro amewaomba wanachama nba wafuasi wa CUF jijini Dar es Salaam kujitokeza kwa wingi kuuga mwili wa Mbunge huyo aliyefikwa na umauti akiwa kazini katika vikao vya Kamati za Bunge, ambapo Marehemu alikuwa Mjumbe wa Kamati ya Bunge ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.
***************************************************************************
Pichani ni Baadhi ya Maofisa wa Ofisi Ndogo ya Bunge,wakimsaidia kwa kumbeba Mbunge wa Chambani,Bwa.SalimHemed Khamis,mara baada ya kuanguka ghafla hapo jana jijini Dar akiwa katika vikao vya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na kukimbizwa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kwa matibabu ya haraka.
======= ====== ======
Habari zilizoifikia Globu ya Jamii hivi punde inaelezwa kuwa aliyekuwa Mbunge wa jimbo la Chambani-Pemba, Salim Hemed Khamis,ambaye hapo jana alianguka ghafla jijini Dar Es Salaam alipokuwa akihudhuria vikao vya kamati ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na kukimbizwa hospitali ya Taifa Muhimbili kwa matibabu, amefariki dunia muda mfupi uliopita katika Hospitali hiyo ya Taifa ya Muhimbili,aidha chanzo cha habari hizi kimeongeza kuwa taratibu za kuusafirisha mwili wa Marehemu kuelekea Pemba kwa mazishi zinafanyika.Tutazidi kuwafahamisha zaidi kadiri ya habari zitakavyokuwa zikiingia.
Mungu ailaze Roho ya Marehemu mahali pema Peponi-Amin
***************************************
WADAU NINA SWALI. Hivi huko Bungeni, hakuna Stretcher ya kubeba wagonjwa? Je, hakuna watu wa First Aid? Hii ni mwaka 2013, wanatakiwa wawe na wahudumu wa afya, ambulance, wahudumu onsite. Watu wawepo wanaoelewa jinsi ya kubeba wagonjwa. Na hasa huko Bungeni waBunge wengi wana umri mkubwa na matatatizo ya kiafya. - Chemi
Tuesday, September 27, 2011
Tanzia - Mama Wangari Maathai (Mama Miti)
Mama Wangari Maathai (1940-2011) |
Mama Maathai alipigania haki za akina mama na maskini nchini Kenya. Alitunga vitabu kadhaa. Alikuwa mwanamke wa kwanza Afrika Mashariki kupata Ph.D katika sayansi za biolojia. Alipoona jangwa inazidi kukuwa nchini Kenya alianzisha mradi wa kupanda miti ili kuepuka janga hilo na hasa kuanzishwa kwa Green Belt Movement. Aliwahi kuwa Mbunge Kenya na pia alifungwa mara kadhaa kutokana na msimamo wake mkaliw wa kutunza ardhi ambayo mara nyingi ilipingana na serikali ya Kenya.
Mungu ailaze roho yake mahala pema mbinguni. Amen.
Kwa habari zaidi BOFYA HAPA:
Labels:
Green Belt Movement,
Kenya,
Mbunge,
Nobel Prize,
Parliament,
Ph.D,
Wangari Maathai
Subscribe to:
Posts (Atom)