Saturday, March 11, 2017
Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi Maliasili na Utallii Yatembela Eneo lenye Mgogoro la Por Tengefu la Loliondo
Wednesday, March 01, 2017
Friday, March 20, 2015
Muswada Binafsi wa Baraza la Vijana la Taifa Kujadiliwa Bungeni
Mh. John Mnyika |
Saturday, October 25, 2014
Mh. Shy-Rose Bhanji Ajibu Shutuma Dhidi Yake
Mh. Shy-Rose Bhanji |
Shy-Rose Bhanji
Mbunge EALA
Tuesday, March 11, 2014
Saturday, March 01, 2014
Mh. Shy-Rose Bhanji Aiomba Serikali ya Tanzania Kuwezesha WaTanzania Waifahamu EAC na Faida Zake
Katibu wa Wabunge wa Tanzania Katika Bunge la Afrika Mashariki, Mhe. Shy-Rose Bhanji (pichani) amerejea nchini baada ya ziara ya siku 10 ya Wabunge wa EALA nchini Kenya na hicho ndicho alichokisema kwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Nimerejea nchini baada ya ziara ya siku 10 nchini Kenya. Ziara hii ya wabunge wa EALA ilikuwa kwa mwaliko wa Serikali ya Kenya lengo likiwa kuhamasisha wananchi wa Kenya kupata ufahamu mkubwa juu ya Mtangamano wa Jumuiya na faida zake. Tulipata nafasi ya kuonana na wananchi, wafanyabiashara, wabunge, maseneta, magavana, asasi za kiraia na makundi mengine.
Ziara hii imenifungua macho zaidi kwamba bado tuna kazi kubwa mbele yetu kuhakikisha kuwa Jumuiya ya Afrika Mashariki inakuwa ni ya Wananchi (people Centred Integration).
Kama nilivojionea mwenyewe kwa upande wa maeneo mbalimbali tuliyoyafikia bado mwamko wa ufahamu wa masuala ya EAC mdogo sana na kiu wa kuifahamu ni kubwa.
Hata hivyo Serikali ya Kenya kwa kuhakikisha wananchi wengi zaidi wanashiriki kikamilifu juu ya masuala ya Jumuiya imefufua mpango huu wa wabunge wa EALA kufika Kenya kuendelea na zoezi la uhamasishaji.
Ni imani yangu kwamba na Serikali ya Tanzania itaiga mfano huu mzuri wa kuwaalika wabunge wa EALA kufika nchini ili kuwafikia makundi mbalimbali hapa nchini kwa lengo la kuhamasisha. Hata kwa upande wa Tz bado ufahamu wa wananchi wengi zaidi juu ya masuala ya Integration ni changamoto kubwa.
Lengo kuu la uanzishwaji wa EAC ni kuinua hali ya kiuchumi kwa wananchi wa EA ambao sasa ni takriban millioni 140. Na iwapo mwamko wa wananchi ni mdogo basi lengo hili litachukua muda mrefu sana kufikiwa au kutokufikiwa kabisa.
Thursday, January 17, 2013
Wenye Hasira Kenya Wachoma Majeneza 221 - Yawakilisha Wabunge
Mshahara wa mbunge Kenya ni $170,000 kwa mwaka! Walitaka wapatiwe bonasi ya $110,000. Huko kipato cha wastani wa Kenya ni $1,700! Hebu linganisha na Marekani. Mbunge anapata $150,000 kabla ya kukatwa kodi. Kipato cha wastani kwa Mwananchi wa Marekani ni $45-50,000/-. Lazima wakasirike!
********************************************************
Kutoka Yahoo News
NAIROBI, Kenya (AP) — Hundreds of demonstrators angered at the conduct of outgoing Kenyan legislators doused 221 coffins with gasoline and set them on fire Wednesday, causing an inferno outside parliament's main entrance.
Organizers of the protest said the coffins represented the end of an era of parliament's 221 legislators and burning the coffins symbolized the start of a new era away from the dishonorable acts that parliament was known for in the last five years. The legislators' term ended earlier this week. Police looked on as the caskets made of thin wood burned to ashes as protesters shouted and screamed in exhilaration.
"Bye bye parasites," shouted Sheldon Ochieng, 23, a college student studying community development. "MP's do not know their work; they are just stashing money in their pockets. It is time to have new leaders who serve the people."
Kenyans say their legislators are seen as lazy, greedy and self-centered for often improving their welfare lavishly at the cost of tax payers. A Kenya legislator earns about $175,000 a year in a country where the average annual income is $1,700. Last week Kenyan legislators attempted to award themselves a $110,000 bonus, but the president vetoed the legislation.
The package would also provide legislators with an armed guard, a diplomatic passport, and access to the VIP lounge at Kenyan airports and state funerals.
It was the second time the President Mwai Kibaki had refused to sign the bill adding the legislators' bonuses into law. In October members of parliament quietly awarded themselves the bonuses.
However, civil society activists say Kibaki, who is the 222nd legislator, is no different from other parliamentarian's because while he vetoed the hefty raises, he has approved hefty increments to a send-off package for when he retires after two terms in office following the country's March 4 elections.
The organizers of the protests Wednesday said they did not make a coffin for the president because of the veto, and the decision to give himself more money came after the coffins had been ordered.
"It was unsurprising that President Kibaki, while rejecting the MPs' pay deal, retained his own hefty retirement package. Moreover, the failure of his administration to rein in grand corruption remains a blot on what many see as credible efforts to grow the country's economy," said Boniface Mwangi, an official of a lobby group called Kenya Ni Kwetu, or Kenya is Our Home.
Atsango Chesoni, the executive director of the Kenya Human Rights Commission, said Monday that the president had contravened the constitution by approving the law that awards him hefty pension increments.
Chesoni said under the constitution Kenya adopted in 2010, the Salaries and Remuneration Commission is the authority charged with rationalizing and deciding the pay for public servants.
Mwalimu Mati, an anti-corruption activist, said the common argument from legislators is that they deserve pay increases because they have passed more bills. Mati said that argument is without merit. He said that although many laws have been crafted during the current parliamentary term, most of the legislation was passed without scrutiny due to low attendance at parliament.
Mati said the legislators spent a lot of time voting on bills for their own benefit, "like watering down sections of the integrity laws which would have required them to declare wealth." The legislators reduced academic qualifications required for one to be elected that were set out after country adopted the constitution in 2010, Mati said.
Friday, January 11, 2013
Wabunge wa WaKenya Wajipandishia Mishahara na Marupurupu!
Nadhani watu watauanua kuwa wabunge Kenya sasa maana hiyo 'package' ya mbunge ni nzito!
***********************************************************
Kutoka BBC.COM
10 January 2013
Kenyan MPs Vote Themselves $100,000 Retirement Bonus
MPs in Kenya have awarded themselves a $107,000 (£65,000) retirement bonus in one of the last sessions of parliament before a general election in March.
The package will also provide them with an armed guard, a diplomatic passport and access to airport VIP lounges.
It is the second time the MPs have voted for "a golden handshake" - President Mwai Kibaki vetoed an attempt last year after widespread protests.
The MPs are among the highest paid in Africa, earning $13,000 a month.
The average yearly salary in Kenya is about $1,700.
The latest vote was passed on Wednesday with fewer than 30 MPs in the chamber - itself refurbished at a cost of $12m last year - according to parliamentary transcripts released on Thursday.
The retirement package is the same as that approved in October, but this time the MPs have also recommended bonuses for the president - almost $300,000 in cash and allowances - the vice-president and the prime minister.
When he vetoed the previous bill, Mr Kibaki said it was "untenable in the prevailing economic circumstances in the country".
The Salaries Review Commission told Kenyan media it was uncertain whether the vote was constitutional, while civil society groups have reacted with outrage.
The executive director of Kenya's Human Rights Commission. Atsango Chesoni, said the package was "preposterous and in completely bad taste".
During its term, the Kenyan parliament repeatedly dismissed the wage demands of striking public sector workers, arguing that the funds were not available.
Sunday, April 01, 2012
Thursday, February 02, 2012
Ikulu Yakana Kuidhinisha Posho za Wabunge
habari zenye kichwa cha habari – JK abariki posho mpya za Wabunge:
Kila mmoja kulipwa sh 330,000 kwa siku.
Habari hizi siyo za kweli na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais inataka
kutoa ufafanuzi ufuatao:
Maelekezo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Jakaya
Mrisho Kikwete kuhusu suala hili yako wazi kabisa na hakuna mahali
ambako Rais Kikwete amebariki posho hizi.
Maelekezo ya Mheshimiwa Rais kuhusu suala hili ni kama ifuatavyo:
Kwanza, Mheshimiwa Rais Kikwete anakubali haja ya kuangalia upya posho
kwa Wabunge lakini amewataka wabunge kutumia hekima na busara katika
kulitafakari suala hili.
Pili, Mheshimiwa Rais Kikwete amewataka Wabunge kutumia Kikao cha sasa
cha Bunge kulizungumza upya suala hilo.
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu.
Dar es Salaam.
31 Januari, 2012
Monday, October 24, 2011
‘Rushwa ya Ngono Inatumika Kupata Ubunge’
***************************************************
Kutoka Gazeti la Habari Leo.
UTAFUTAJI wa vyeo kama ubunge na vingine vya maofisini miongoni mwa wanawake wasiojiamini, ni sababu kubwa ya kuendelea kuwepo kwa rushwa ya ngono nchini.
Aidha, imeelezwa kuwa matumizi mabaya ya madaraka yanayofanywa na baadhi ya wanaume ni kichocheo kingine cha rushwa hiyo, inayochangia nchi kuwa na viongozi wasio na uwezo, maadili mema, kwa asilimia kubwa.
Akizungumza wakati wa mkutano wa Kamati ya Bunge ya masuala ya Ukimwi iliyokutana Dar es Salaam mwishoni mwa wiki, kujielimisha kuhusu unyanyasaji wa jinsia nchini, Mbunge wa Viti Maalum, Hilda Ngoye (CCM) alisema rushwa hiyo ipo na inarindima hata kwa wabunge.
Huku akiungwa mkono na Waziri Kivuli wa Afya na Ustawi wa Jamii, ambaye pia ni Mbunge wa Biharamulo Magharibi (CHADEMA), Dk.Gervas Mbassa, Ngoye alisema anachokizungumza kinafanyika si tu katika kuutafuta ubunge, bali hata katika kutafuta vyeo maofisini.
Wakati akisema hayo, Mbunge wa Viti Maalu, Margret Mkanga (CCM) alishtuka kwa mshangao ulioashiria kuisikia habari hiyo kwa mara ya kwaza na ndipo Ngoye alipomwambia, “Usishangae! It is a practical example, akimaanisha kuwa alichokizungumza ni mfano hai uliopo.
Kwa upande wake, Mbassa aliliambia gazeti hili kuwa hali hiyo ipo kweli na kwamba inatokana na kukosa utu miongoni mwa wanaoomba na wanaotoa rushwa ya ngono.
Alisema, wengi wanaojihusisha na rushwa hiyo na kushindwa kupata wanachokitaka huishia kuaibika au kupata maambukizi ya VVU huku walioigawa na kuupata uongozi wakiiharibu nchi kwa njia tofauti kutokana na kukosa maadili ya uongozi pamoja na uwezo wa kazi.
“Alichokisema Ngoye ni sahihi kabisa, rushwa ya ngono ipo hata kwa wabunge. Lakini pia ipo katika nyanja zingine ambazo si za siasa. Watu wanataka uongozi wakati wanajua hawana uwezo na matokeo yake wanaamua kutumia miili yao.
“Ufike wakati Watanzania tuikatae na kuthamini utu vinginevyo nchi itajaa viongozi watakaotusababishia matokeo mabaya,” Ndassa alisema.
Wakati huo huo, baadhi ya wabunge wanaounda kamati hiyo wamewataka wanafunzi wanaoombwa rushwa ya ngono kutoa taarifa kwa maofisa wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) ili wahusika wakamatwe na kushitakiwa, kwa sababu kitendo hicho, licha ya kuwa kosa la jinai, kinatumiwa na wengi kusambaza VVU.
Mbunge wa Viti Maalum, Rosweeta Kasikila (CCM) na Mbunge wa Kilindi, Beatrice Shelukindo (CCM), walisema hayo kwa nyakati tofauti wakati wakitoa michango yao, kuhusu unyanyasaji wa kijinsia, unaohusisha ngono nchini.
Kasikila ambaye ni Kaimu Mwenyekiti wa Kamati hiyo, alisema kuwa wanafunzi ni waathirika wakubwa wa rushwa ya ngono na kwamba wanahitaji kupewa elimu zaidi juu ya athari za rushwa hiyo ya ngono kwa watu mbalimbali wanaowarubuni ili waikatae na kuwaripoti wanaowashawishi kuishiriki.
“Wapo wasichana na hata wavulana jasiri wanaowaeleza maofisa wa Takukuru kuhusu kuombwa rushwa ya ngono na hivyo kuandaa mitego inayowezesha kunaswa kwa wengi wao na kushitakiwa.
Hiyo ni njia mojawapo inayoweza kusaidia kupunguza kuenea kwa maambukizi ya VVU ambayo wengi wao huyapata wanaposhiriki kujamiiana huko”, Kasikila alisema.
Naye Shelukindo alisema kuwa wanafunzi wanastahili kujengewa ujasiri wa kuwaeleza wakubwa wao na taasisi zinazoshughulikia masuala ya haki zao ili kukomesha vitendo vya unyanyasaji vinavyofanywa dhidi yao, kama vile kuhisishwa katika masuala ya kujamiiana kwa kurubuniwa kupata wanachokihitaji.
Alisema, rushwa ya ngono haistahili kuwepo mahali popote pale kwa kuwa ni njia mojawapo inayochochea maambukizi kutokana na ukweli kuwa mara nyingi wahusika wanaoishiriki hawapati muda au kukumbuka
CHANZO: Gazeti la Habari Leo
Thursday, August 11, 2011
MBunge Adai Naibu Spika Mhe. Job Ndugai Ameshindwa Kuendesha vikao vya Bunge
Leo tarehe 11 Agosti 2011 katika kikao cha 48 cha Mkutano wa Nne wa Bunge la Kumi nilitaka kuomba muongozo wa Spika kwa mujibu wa Kanuni za Kudumu za Bunge (Toleo la 2007 ) kifungu cha 68 (7) kuhusu maswali na majibu ya Waziri Mkuu na nikarejea pia kanuni ya 133 (1).
Hata hivyo, kabla hata ya kutoa maelezo kamili ya kuomba muongozo wa Spika nilizuiwa na Naibu Spika Mheshimiwa Job Ndugai (Mb) bila hata ya kusikilizwa muongozo ambao nilitaka kuomba kinyume na kanuni ya 5 (1) inayotaka Spika kuongoza Bunge kwa kuzingatia kanuni na pale ambapo kanuni hazijatoa muongozo Spika anapaswa kufanya kazi kwa kuzingatia katiba, sheria nyingine za nchi, kanuni nyingine zilizopo, maamuzi ya awali na desturi za kibunge.
Naomba kutoa taarifa kwa umma kwamba sijaridhika na uamuzi uliofanywa na Naibu Spika Mheshimiwa Job Ndugai hivyo nawajulisha kwamba ninakusudia kuwasilisha malalamiko kwa mujibu wa kanuni za Bunge kifungu 5 (4) na 7 (3) mara baada ya kupata nakala ya kumbukumbu rasmi ya Bunge (Hansard) ya kikao husika.
Mara baada ya kunukuu kanuni husika nilipoanza tu kuzungumza kwamba katika kipindi cha Maswali na Majibu kwa Waziri Mkuu, Waziri Mkuu Mizengo Pinda amekuwa akitoa majibu yenye upotoshaji yasiyokuwa ya kweli; baada ya kauli hiyo kabla hata ya kumaliza maelezo niweze kuomba muongozo kwa Spika; Naibu Spika alinikatisha na kuninyima fursa ya kuomba muongozo kinyume na kifungu 68 (7) na 5 (1).
Naomba umma uelewe kwamba nilikuwa naelewa kwa kina mahitaji ya kanuni za bunge kifungu cha 133 na vipengele vyake kuanzia cha kwanza mpaka cha sita; ndio maana katika kuanza kuomba muongozo nikasoma kifungu cha 133(1).
Napenda umma ufahamu kwamba muongozo ambao nilitaka kuomba kwa Spika ni kwamba kumekuwa na kawaida ya Waziri Mkuu wakati akijibu maswali ya papo kwa papo kutoa maelezo yasiyokuwa ya kweli yenye upotoshaji ambayo ni kinyume cha katiba ya nchi, sheria mbalimbali pamoja na kanuni ikiwemo kanuni za bunge hivyo nilitaka Spika atoe muongozo wenye kumpa nafasi nyingine Waziri Mkuu kutoa ufafanuzi wa kweli kuhusu masuala husika ili kuepusha uwezekano wa wabunge kupoteza imani na Waziri Mkuu kwa mujibu wa kanuni za bunge kifungu cha 133.
Katika maelezo yangu ya kuomba muongozo huo nilikusudia kutaja mifano miwili mikubwa ya majibu ya Waziri Mkuu kwenye maswali ya papo kwa papo yasiyokuwa ya kweli yenye upotoshaji kuhusu kashfa ya Meremeta na kuhusu mgogoro katika Manispaa ya Arusha.
Ikumbukwe kwamba tarehe 14 Aprili 2011 wakati wa kikao cha saba cha mkutano wa tatu wa Bunge la Tanzania wakati wa maswali ya papo kwa papo kwa Waziri Mkuu, nilimuuliza Mheshimiwa Mizengo Pinda kuwa “Rais Jakaya Mrisho Kikwete, ambaye vile vile ni Mwenyekiti wa CCM amenukuliwa akizungumzia kuhusu haja ya Chama kinachotawala kujivua gamba. Kati ya mambo aliyoyazungumza ni pamoja na kuondokana na watuhumiwa wa ufisadi. Mheshimiwa Mkuu uliwahi kulieleza Bunge hili tukufu kwamba usingetaka kabisa kuzungumzia masuala ya Meremeta kwa sababu ni siri za Jeshi. Baada ya kauli hii ya Rais na dhamira hii ya kujivua gamba kuhusiana na masuala ya ufisadi. Je, uko tayari Mheshimiwa Waziri Mkuu kutaja wahusika wa Kampuni ya Meremeta na kuelekeza Serikali kuchukua hatua zinazostahili kuhusiana na tuhuma hizo? . Waziri Mkuu katika majibu yake Mheshimiwa Mizengo Pinda hakuitumia nafasi hiyo kurekebisha kauli zake zisizokuwa za kweli zenye upotoshaji alizozitoa kwa nyakati mbalimbali katika Bunge la Tisa kuhusu kashfa ya Meremeta.
Ikumbukwe pia kwamba tarehe 10 Februari 2011 katika kikao cha tatu cha mkutano wa pili wa Bunge la kumi Waziri Mkuu Mizengo Pinda akijibu maswali ya papo kwa papo ya Mheshimiwa Freeman Mbowe (Mb) kuhusu matukio yaliyojitokeza Arusha wakati na baada ya uchaguzi batili wa Meya wa Halmashauri ya Jiji la Arusha. Tarehe 11 Agosti 2011 katika kipindi cha Maswali ya papo kwa papo ya Waziri Mkuu kuliulizwa maswali kuhusu maamuzi ya kikao cha Kamati Kuu ya CHADEMA ya tarehe 6 na 7 Agosti 2011 kwa kurejea pia mazungumzo baina ya Waziri Mkuu na viongozi wa taifa CHADEMA kuhusu muafaka batili juu ya mgogoro katika Halmashauri ya Jiji la Arusha na uamuzi wa kuwafukuza uanachama madiwani watano kutokana na kukiuka maagizo ya kamati kuu. Badala ya Waziri Mkuu kuitumia nafasi hiyo kutoa majibu yenye kulenga kutoa ufafanuzi wa kurekebisha upotoshaji uliofanyika awali Waziri Mkuu Mizengo Pinda akatoa majibu mengine yasiyokuwa ya kweli kuhusu mazungumzo yake na viongozi wa CHADEMA pamoja na uamuzi wa chama wa kuwafukuza uanachama madiwani waliokiuka maamuzi ya kamati kuu ya chama.
Majibu ya Waziri Mkuu kuhusu ufisadi wa Meremeta, matukio katika halmashauri ya Jiji la Arusha na masuala mengine ya kitaifa katika kipindi cha maswali ya papo kwa papo yenye uhusiano na utekelezaji wa majukumu ya Waziri Mkuu yaliyoanishwa katika ibara ya 52 ya katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania yana mwelekeo wa kuvunja sheria ya maadili ya viongozi wa umma, sheria nyingine za nchi yetu pamoja na misingi muhimu ya utawala bora kama ambavyo nitafafanua katika hatua zinazofuata. Naomba umma upuuze upotoshaji uliofanywa na Naibu Spika Job Ndugai kuhusu muongozo nilioomba mpaka pale maamuzi yatakapofanywa na Kamati ya Kanuni za Bunge kwa mujibu wa kifungu 5(5) na Bunge kujulishwa.
Wenu katika utumishi wa umma,
John Mnyika (Mb)
Bungeni-Dodoma
11/08/2011
Tuesday, August 09, 2011
Tamko Rasmi la Waziri wa Nishati na Madini Bungeni Kuhusu Upatakanaji wa Mafuta Nchini
TAREHE 9 AGOSTI 2011, DODOMA
Mheshimiwa Spika,
Awali ya yote napenda kuchukua nafasi hii kulishukuru Bunge lako tukufu kwa kunipa fursa hii ya kutoa taarifa kuhusu hali ya biashara ya mafuta ya petroli hapa nchini.
Kama tunavyofahamu, mafuta ya petroli ni muhimu sana kwa uchumi wa nchi yetu kwani viwanda, vyombo vya usafiri, na huduma nyinginezo nyingi hutegemea mafuta na bidhaa zake. Bei ya mafuta inapopanda, bei zingine nyingi hupanda kwa mfano bei za usafiri zinapanda, bei za vyakula zinapanda, bei za bidhaa za viwandani zinapanda; nakadhalika.
Mheshimiwa Spika, tarehe 22 Juni 2011 Serikali, kupitia kwa Waziri wa Fedha wakati akihitimisha Hotuba ya Bajeti ya Serikali kwa mwaka 2011/12, alitoa maagizo kwa Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati na Maji (EWURA) kuchukua hatua mbalimbali zitakazochangia kupunguza bei za mafuta. Hatua ambazo ziliagizwa kuchukuliwa ni pamoja na:
Ukokotoaji wa thamani ya shilingi kwa kuioanisha na Dola ya Marekani (yaani Exchange rate);
Kuondoa au kupunguza wigo wa asilimia 7.5 ambayo makampuni yaliruhusiwa kuwekwa ili kufidia baadhi ya gharama;
kupitia upya misingi ya ukokotoaji wa viwango vya tozo mbalimbali za taasisi za Umma kwa lengo la kubakia na tozo stahili na kwa viwango stahili bila kuathiri majukumu ya udhibiti ma usimamizi yanayofanywa na Taasisi hizo;
kupunguza tozo za kampuni za mafuta ikiwa ni pamoja na gharama za kibenki (yaani Financiang Charges); na
Upotevu wa mafuta yanayosafirishwa kwenye meli na gharama ya ukaguzi (yaani inspection fee).
HATUA ZILIZOCHUKULIWA NA SERIKALI
Serikali kupitia EWURA ilianza mara moja mchakato wa kurekebisha Kanuni ya ukokotoaji wa bei za mafuta hapa nchini kwa lengo la kuleta unafuu wa bei kwa mlaji. Hatua ya kwanza ilikuwa kuandaa hoja (discussion paper) ambayo ilitoa mapendekezo ya maeneo mbalimbali yanayofaa kurekebishwa ili kupata maoni ya wadau wa sekta ya mafuta. Mapendekezo hayo yalizingatia maagizo ya Serikali pamoja wa ushauri mbalimbali wa wadau katika sekta ya mafuta hapa nchini.
USHIRIKISHAJI WADAU
Mchakato wa kupata maoni ya wadau (taftishi) ulianza tarehe 4 Julai 2011 na kukamilika tarehe 26 Julai 2011. Kwa kawaida, mchakato huo ungechukua siku 81 lakini kutokana na unyeti wa suala hili, Mamlaka ililazimika kuufupisha hadi siku 23.
Mkutano wadau uliitishwa tarehe 22 Julai 2011 ili kupitia rasimu ya kanuni pamoja na jedwali la uchambuzi wa maoni ya wadau lililoandaliwa na EWURA. Wadau walioshirikishwa katika taftishi hiyo ni pamoja na makampuni ya mafuta, Baraza la Watumiaji wa Huduma zinazodhibitiwa na EWURA (Consumer Consultative Council), Baraza la Ushauri la Serikali, Taasisi za Umma kama vile TRA, TBS, WMA, TPDC, TPA, SUMATRA, na TIPER. Maoni mbalimbali ya wadau yalipokelewa na kuchambuliwa na EWURA ikiwa ni pamoja na kupata maoni ya wataalam kutoka taasisi mbalimbali zikiwemo Wizara ya Nishati na Madini, Wizara ya Fedha na Uchumi, Shirika la Maendeleo ya Mfuta Tanzania (TPDC), Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, EWURA na Makampuni ya Mafuta.
Tarehe 23 Julai 2011, EWURA iliitisha kikao cha wawakilishi wa wadau wakubwa ambao ni pamoja na CCC, TPDC, TPA, Wizara ya Nishati na Madini, Mwanasheria Mkuu na baadhi ya makampuni ya mafuta kupitia mapendekezo yaliyokuwepo na kutoa maoni ya mwisho kabla ya kuwasilishwa kwenye Bodi kwa maamuzi.
MAAMUZI YA EWURA
Tarehe 26 Julai 2011, Bodi ya Wakurugenzi ya EWURA ilikaa na kupitia mapendekezo ya marekebisho ya vipengele mbalimbali vya kanuni ya kukokotoa bei ya mafuta. Maamuzi hayo ya Bodi yamepelekea punguzo la bei za mafuta kwa viwango vifuatavyo: Petroli TZS 202.37; Dizeli TZS 173.49; na Mafuta ya Taa TZS 181.37. Mabadiliko haya ya bei ni sawa na punguzo la asilimia 9.17; 8.31; na 8.70 kwa mafuta ya petroli, dizeli na mafuta ya taa sawia. Kanuni hii ya kukokotoa bei za mafuta imeanza kutekelezwa kuanzia tarehe 03 Agosti 2011.
Tarehe 3 na 4 Agosti 2011 makampuni ya mafuta yaliwasilisha kutoridhishwa na maamuzi yaliyofanywa na EWURA hususan kuhusu kupunguzwa kwa wigo wa asilimia 7.5; margins za makampuni ya mafuta, na gharama za kuchelewesha meli bandarini (demmurage charges).
Kufuatia vikao hivyo vya Serikali, makampuni pamoja na EWURA siku ya Ijumaa tarehe 5 Agosti 2011, Mamlaka ya EWURA ilifanya marekebisho mengine katika vipengele vifuatavyo:
Gharama za ucheleweshaji meli bandarini (demmurage charges) ziliongezwa kutoka wastani wa TZS 1.85 kwa lita hadi TZS 8.76 kwa lita.
Viwango vya faida kwa kampuni za mafuta (OMCs margins) ziliongezwa kutoka TZS 108.69 kwa lita hadi TZS 110.57.
HALI YA UPATIKANAJI NA USAMBAZAJI MAFUTA BAADA YA KUANZA KUTUMIKA KWA KANUNI MPYA
Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) kwa kushirikiana na Wizara ya Nishati na Madini imeendelea kufuatilia kwa karibu mwenendo wa bishara ya mafuta hapa nchini. Ufuatiliaji uliofanywa kwenye maghala ya kuhifadhia mafuta umedhihirisha kuwa kuna mafuta ya kutosha hapa nchini na pia kuna meli kadhaa ambazo zipo nje ya gati zikisubiri kupakua mafuta. Aidha, makampuni ya mafuta yameuza mafuta kwa wingi siku ya Ijumaa tarehe 5 Agosti 2011.
Hadi Ijumaa tarehe 05.08.2011, kiasi cha mafuta yaliyokuwepo katika maghala ya baadhi ya makampuni ya mafuta yaliyokaguliwa ni lita milioni 191.813 ambayo inakidhi matumizi ya nchi kwa kati ya siku 8 hadi 67 kulingana na aina ya mafuta kama inavyoonekana kwenye jedwali Na. 1 hapa chini:
Jedwali 1: Mafuta yaliyoko Nchini tarehe 05 Agosti 2011
Maelezo Mafuta ya Petroli Mafuta ya Dizeli Mafuta ya Taa Mafuta ya Ndege Mafuta Mazito
Akiba iliyopo(lita) 41,934,139 92,650,300 41,227,870 4,384,297 10,805,070
Wastani wa Matumizi kwa siku 875,000 3,100,000 615,240 560,500 1,087,695
Makadirio ya siku za kutumika 48 30 67 8 TAMKO LA WAZIRI WA NISHATI NA MADINI KWA BUNGE LA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA KUHUSU UPATIKANAJI WA MAFUTA NCHINI

10
MAUZO YA MAFUTA KWENYE MAGHALA (JUMLA)
Takwimu zilizowasilishwa EWURA na mkandarasi anayeweka vinasaba katika mafuta yauzwayo hapa nchini (GFI) na kuhakikiwa na wakaguzi wa EWURA zinaonesha kuwa kwa siku ya Ijumaa tarehe 5 Agosti 2011 mauzo ya mafuta kutoka kwenye maghala (depots) yalikuwa ni malori 329 kwa aina mbalimbali za mafuta, kwa ajili ya soko la ndani.
Tarehe 3 Agosti walipakia malori 40 wakati tarehe 4 Agosti 2011 yalipakiwa malori 185. Kwa kawaida, wastani wa mauzo kwa siku ni takriban malori 250 hadi 300. Takwimu hizi zinadhihirisha kuwa kuanzia tarehe 5 Agosti 2011, mauzo ya mafuta yameongezeka na kufikia kiwango cha kawaida.
Katika hali ya kawaida, makampuni mengi ya mafuta hayafanyi kazi katika siku za mapumziko. Kwa hiyo, siku ya Jumamosi tarehe 6 Agosti 2011, jumla ya malori 115 yalipakia mafuta.
MAUZO YA MAFUTA KWENYE VITUO (REJAREJA)
Ukaguzi uliofanywa na EWURA kwenye vituo vya mafuta jijini Dar es Salaam na baadhi ya mikoa unaonesha kuwa vituo vingi vilianza kuuza mafuta kama kawaida. Ukaguzi huo pia umehusisha kupata takwimu za mafuta yaliyopo kwenye vituo ili kuhakikisha kuwa hakuna kituo kinachohodhi mafuta na kuacha kuuza. Kuna baadhi ya vituo vilikuwa vikisubiri kupata mafuta kwa vile walikuwa wameishiwa, hasa kwa sababu makampuni ya mafuta hayakuuza mafuta kwa kiwango cha kawaida siku ya tarehe 3 na 4 Agosti 2011.
Makampuni mengi yaliendelea kupakia malori ya mafuta mpaka usiku 5 Agosti 2011 hivyo ilitarajiwa kwamba kungekuwa na usambazaji mwingi zaidi kwenye vituo kuanzia Jumamosi tarehe 6 Agosti 2011.
VIWANGO VYA BEI
Ukaguzi uliofanywa na EWURA unaonesha kuwa bei za mafuta kwenye vituo vinavyouza mafuta zimezingatia bei kikomo zilizotolewa na Mamlaka ya EWURA tarehe 3 Agosti 2011. Ukaguzi huo umefanyika katika miji ya Arusha, Moshi, Dar es Salaam na Dodoma. Aidha, hakuna taarifa zilizopokewa na EWURA kutoka mji wowote kuhusu kukiukwa kwa bei kikomo iliyopo sasa.
HATUA ZINAZOCHUKULIWA NA SERIKALI
Mheshimiwa Spika, bidhaa za mafuta ya petroli inatoa mchango mkubwa katika kukuza uchumi katika nchi zote duniani. Upatikanaji wa uhakika wa mafuta na kwa bei stahili vitafanya uchumi wa nchi yetu kukua kwa kasi zaidi na kuwa endelevu.
Serikali inachukua hatua zifuatazo ili kuhakikisha kuwa mafuta ya kutosha yanapatikana sehemu zote nchini.
Serikali kupitia EWURA inafuatilia mwenendo wa usambazaji wa mafuta kutoka katika maghala ya makampuni ya mafuta kwenda kwenye vituo vya mafuta;
Serikali kupitia EWURA itachukua hatua za kisheria kwa kampuni zilizokiuka masharti ya leseni na kusababisha uhaba wa mafuta kwenye vituo vya kuuza mafuta nchini;
Leo Serikali kupitia EWURA imeipa leseni COPEC kampuni tanzu ya Serikali kupitia TPDC kuanza kufanya biashara ya mafuta mara moja; na
Serikali kwa kupitia EWURA imekamilisha taratibu za uagizaji wa mafuta kwa pamoja ili kuhakikisha kuwa mafuta yanapatika na kwa gharama nafuu zaidi wakati wote.
Mheshimiwa Spika, kufuatia hali iliyojitokeza, EWURA imetoa Compliance Order kwa makampuni manne ambayo ni BP, Engen, Oilcom na Camel Oil, ambapo wanatakiwa watekeleze hatua zifuatazo:
Mara moja wanatakiwa kuanza kutoa huduma katika maghala yao ikiwa ni pamoja na kuanza kuuza mafuta katika vituo vya rejareja ikiwemo vituo vilivyo chini ya miliki zao;
Waache mara moja kitendo chochote kitakachosababisha upungufu wa makusudi wa mafuta ya petroli katika soko la Tanzania; na katika kipindi cha masaa 24 wajieleze kwa nini wasichukuliwe hatua za kisheria dhidi yao kwa kukiuka matakwa ya Sheria ya Mafuta pamoja na Sheria ya EWURA.
Mheshimiwa Spika, baada ya kuisha kwa muda uliotolewa na EWURA, adhabu stahiki zitatolewa kwa wahusika ikiwa ni pamoja na kusitisha ama kufuta leseni.
Mheshimiwa Spika, katika hali ya kawaida na kwa mujibu wa Sheria, mtu asiporidhika na maamuzi ya EWURA anapaswa kukata rufani katika Baraza la Ushindani (Fair Competition Tribunal). Hatua hii haijafuatwa hadi sasa na Serikali ingeshauri kwamba masuala kama haya ni vema yakafuata taratibu za kisheria.
Mheshimiwa Spika; naomba kuwasilisha.