Showing posts with label Wazazi. Show all posts
Showing posts with label Wazazi. Show all posts

Saturday, November 02, 2019

Leah Mwamoto Awaonya Wazazi wa Kilolo Wanaokatisha Masomo ya Wanafunzi

Mjumbe wa halmashauri Kuu (CCM) Mkoa wa Iringa, Leah Mwamoto akiongea na wazazi wa shule ya sekondari ya Mlafu iliyopo katika wilaya ya Kilolo mkoani Iringa
 Wanafunzi wa shule ya sekondari ya Mlafu iliyopo katika wilaya ya Kilolo mkoani Iringa wakicheza nyimbo mbele ya mgeni Rasmi

NA FREDY MGUNDA,KILOLO

Mjumbe wa halmashauri Kuu (CCM) Mkoa wa Iringa, Leah Mwamoto amewaonya wazazi wanaokatisha masomo watoto kuwa serikali itawachukulia hatua kali pindi watakapobainika kufanya kosa hilo.

Mwamoto ameongea hayo katika mahafali ya kidato cha nne katika shule ya sekondari ya Mlafu iliyopo katika kijiji cha Mlafu wilayani Kilolo alipomuwakilisha mbunge wa jimbo la Kilolo Venance Mwamoto.

Akiwaonya wazazi katika mahafali hayo Mwamoto amewaeleza wazazi juu ya mazingira mabaya wanayoyakuta watoto wanaokwenda kufanya kazi za ndani katika miji mikubwa.

Hata hivyo amewaomba watendaji wa kata kuendelea kuwafutilia watoto ili kuwaepusha kujiingiza katika mazingira hatarishi yatakayoharibu ndoto zao.

Aidha Mwamoto amepongeza uongozi wa shule ya sekondari Mlafu kwa matokeo mazuri pamoja na mbunge wa jimbo la Kilolo, Mhe Venance Mwamoto kuchangia bati 180 na mifuko 100 ya saruji kwa ujenzi wa zahanati kijiji cha Mlafu.

Awali akisoma taarifa fupi ya shule mwalimu mkuu wa shule hiyo Emmanuel Mbangwa ameomba wadau kujitokeza kuboresha mazingira katika shule hiyo hususani kujenga nyumba za walimu na mabweni.

Nae diwani Mlafu Isidory Kiyenge amewataka wazazi wa kata hiyo pamoja na wadau kuwa tayari kuchangia katika sekta ya elimu ili kuongeza mazingira ya ufaulu.

Kayenge amewataka wanafunzi kujiandaa kwa mitihani ya kidato cha nne huku alito ahadi ya kuwaandalia chakula wakati wa mitihani.

Thursday, April 12, 2012

Baba Lulu Aongea na Waandishi wa Habari

KWA HISANI YA BLOGU YA JAMII:

Mzee Michael Edward Kimemeta (picha na Dixon Busagaga)

Imeandikwa n Dixon Busagaga  - Globu ya Jamii Moshi


Baba mzazi wa Muigizaji wa kike wa filami nchini maarufu kama Lulu, ambaye anahusishwa na kifo cha marehemu Steven Charles Kanumba, ameibuka na kueleza kushtushwa sana na taarifa za kifo hicho pamoja na habari kuwa bintiye alikuwa na mahusiano ya kimapenzi na muigizaji huyo nguli na kuwa anahusika na kifo chake.

 Baba Lulu, ambaye alijitambulisha kwa jina la Michael Edward Kimemeta(49) mzaliwa wa Wilaya ya Rombo, Mkoani Kilimanjaro, kaiambia Globu ya Jamii leo huko Moshi kuwa alimtambua Steven Kanumba kama mwalimu wa mtoto wake Lulu,lakini hakuamini masikio yake baada ya kupata taarifa za kifo hicho, huku bintiye, anayedaiwa alikuwa na mahusiano ya kimapenzi na marehemu, anahusika.


Lulu alifikishwa mahakamani jana April 11, 2012 akikabiriwa na mashtaka ya mauaji ya Marehemu Steven Kanumba, ikiwa ni siku nne baada ya kifo cha msanii huyo. Alisema kuwa Elizabeth ama Lulu alizaliwa tarehe April 17,1995 katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar es Salaam, na kwamba alimaliza elimu ya kidato cha nne katika shule ya sekondari ya Midway mwaka jana na kamba hivi sasa ana umri wa miaka 17.

Bw Kimemeta alisema kuwa ni vyema polisi kuwa makini katika uchunguzi wao kwa kuzingatia kuwa tukio hilo limejenga chuki na uhasama baina ya Lulu na ndugu, jamaa, marafiki na wapenzi wa marehemu Steven Kanumba. Alisema kuwa kilichomshtusha zaidi ni taarifa za polisi kusema kuwa kulitokea ugomvi kati ya Marehemu Steve Kanumba na Lulu,huku ikitajwa kuwa walikuwa wapenzi.

“Hatukutegemea kama Marehemu Kanumba angeweza kuwa na mahusiano y kimapenzi na binti yetu; kwanza ndiye tuliyekuwa tukimtegemea kwa kiasi kikubwa katika kuendeleza na kukikuza kipaji alichokuwa nacho Elizabeth”, alisema baba mtu. “Ninaomba Wanasheria na wanaharakati wa haki za kibinadamu kuingilia suala hili na kusaidia katika kupatikana kwa haki dhidi ya shtaka la mauaji linalomkabili binti yangu Elizabeth na pia naomba swala hili lisichukuliwe kishabiki ama kwa hisia bali haki ichukue mkondo wake”alisema.

Kanumba na Lulu mwaka jana.  Picha kwa hisani ya  Mpeli Jr Ngonywike
 Alisisitiza kuwa jamii inatakiwa kutambua mazingira ya tukio hilo,ambapo chanzo kinasemekana ni ugomvi uliopelekea tafrani kwa Lulu kutuhumiwa kumsukuma Marehemu Kanumba kwa kile kinachodaiwa kuwa ulikuwa wivu wa kimapepenzi na haiyumkini hakukusidua kumuua hivyo yeye anashangaa bintiye kuhusishwa moja kwa moja na mauaji.

“Ushiriki wa mwanangu kuhusu mambo ya sanaa nilikwishapata wasiwasi na mama yake mzazi alikuwa akiwasiliana na Marehemu Kanumba enzi za uihai wake ambaye alikuwa anamhakikishia usalama wa Lulu na kusema kuwa ataendele kubaki kama mwalimu…..lakini leo nasikia alikuwa ni mpenzi - nilishtushwa” alisema Kimemeta.

Baba Lulu pia ameelezea kusikitishwa kwake kwa kushindwa kuhudhuria mazishi marehemu Steven Kanumba kuhofia usalama wake, na kusema mazingira yatakaporuhusu hata sita kufika nyumbani kwa marehemu Steven Kanumba na kutoa pole. Bw Kimemeta amesema kuwa anaungana na Watanzania wote kutoa pole kwa familia ya Marehemu Steven Kanumba na kutoa mkono wa pole kwa msiba huo mkubwa ambao haukutarajiwa.Kasema kuwa Kanumba alikuwa bado ni kijana mdogo aliyeonyesha umahiri kwenye sanaa na kwamba amecha pengo kwa familia yake na Tanzania kwa ujumla.

Lulu na Mama yake Mzazi, Bi Lucrecia Kalugila

Friday, June 10, 2011

Blogu Mpya - TZ Moms Abroad

Mdau Cyndi ameanzisha blogu:

Nimeanza mda si mrefu. Unakaribishwa pia kunitembelea katika blog yangu ambayo inamatumaini ya kukutanisha akina dada, mama na wanawake kwa ujumla katika kujadili mambo ya kijamii na maisha kwa ujumla. Pia kutoa support kwa wanawake wanaharakati katika jamii na wanabusiness. Anyways, please soma my welcome message to know what tzmomsconnect is all about.

Here is the link: http://tzmomsabroad.blogspot.com/

http://tzmomsabroad.blogspot.com/

Tuesday, March 15, 2011

Mimi katika Mchezo- 'The Vagina Monologues'

Washiriki wa Boston Community Production of The Vagina Monologues 2011

Wikiendi iliyopita nilishiriki katika Mchezo wa Kuigiza, The Vagina Monologues (Maongezi ya Uke ..nishahishe kama nimekosea kutafsiri).

Kila mwaka vikundi vya wanawake hapa Marekani na nchi nyingi duniani wanasoma na kuigiza huo mchezo mwezi Machi. Hela wanazopata kutoka kwenye viingilio na mauzo ya chakula zinakwenda kusaidia vyama, mashirika yanayosaidia akina mama. Machi ni mwezi ya Wanawake duniani.

The Vagina Monologues ni hadithi fupi mbalimbali zinazotokana na mahojiano aliyofanya Bi Eve Ensler na wanawake kadhaa kuhusu nyeti zao. Kulikuwa na maongezi ya Bi Kizee, Shoga, Mke, Uke uliyokasirika, Mwanamke aliyedhani kapoteza kiharage chake, Kubalehe, Kubakwa, Kutairiwa, na mengine.

Kwa kweli nimetokea kufurahia huo mchezo na hata wanaume niliyowaalika waliyoenda wameipenda sana. Imewafanya wafikirie haki za akina mama na pia jinsi akina mama wanavyoona maswala kama uke zao, ngono, kunyanyyawa kijinisia.

Tanzania kuna hadithi nyingi sana ambazo zinaweza kuingizwa katika huo mchezo.

Mnauliza niliongelea nini? Nililionogelea uzazi, jinsi mwanamke anavyokuwa na uchungu katika uzazi na jinsi uke unavyofunguka ili mtoto atoke.

Tuesday, July 03, 2007

Wazazi Wangu safarini Boston

Kutoka Kushoto, Mhesimiwa Frederick Sumaye, Dr. Aleck Che-Mponda, mimi na mama yangu. Tulienda kumsalimia Mheshimwa Sumaye, ambaye kwa kweli alikuwa mkarimu sana. Msaidizi wake alitupikia mishikaki mitamu kama nyumbani. Mheshimiwa Sumaye amemaliza masomo yake Harvard University hivi karibuni.


Baba akiagana na Mheshimiwa Sumaye ambaye alikuwa jirani yangu hapa Cambridge, Ma. Ndo siku nilikabidhi kanda za sinema ya Tusamehe na Bongoland.

Baba na Mama wakiwa South Station, Boston Ma. kuelekea New York City ambapo walienda kusalimia ndugu na marafiki.


Dr. Aleck Che-Mponda akicheki sanamu ya mbwa aina ya St. Bernard huko Mohegan Sun.