Hapa Marekani kuna jimbo inaitwa West Virginia. Hiyo jimbo inajulikana kwa watu washamba sana (hillibiilies). Wanavyosema kwenye milima ya kule ni jambo la kawaida mtu kufunga ndoa na ndugu yake, hatimaye watoto wanakuwa na nyuso za ajabu na hawana akili sana.
Sasa kuna sinema ambayo inaanza kutengenezwa mwezi ujao, inaitwa Shelter. Stelingi wake ni Julianne Moore. Sasa katika kutafuta extras, mtu aliyekabidhiwa hiyo kazi alitangaza casting call ya ajabu.
Donna Belajac Casting iliyoko Pennsylvania ilitangaza kuwa inatafuta, watu warefu mno, watu wafupi, watu wenye shepu za ajabu na uso za ajabu. Walisema pia kuwa wanatafuta watu wenye kasoro kwenye miili yao hasa macho. Pia walikuwa wanatafuta viwete wasiohitaja msaada maalum.
Haya hiyo siyo mbaya, lakini aliharibu aliposema anatafuta watu ambao wanafanana na 'inbred' yaani waliozaliana wenyewe kwa wenyewe. Tena waliongeza watu wanafanana na 'holler people' ni kabila fulani ya ya wazungu wanaokaa kwenye milima ya West Virginia.
Hapo huyo Donna Belajac kawasha moto! Viongozi wa West Virginia walichachamaa maana walisema kuwa ni stereotype kuamini kuwa watu wa West Virginia ni inbreds na washamba! Gavana Joe Manchin wa West Virginia alilaani hiyo sinema na hiyo casting call vikali! Pia viongozi wengine waliingilia.
Mwisho watengeneza sinema ya Shelter, waliomba msamaha kwa watu wa West Virginia na pia walifukuza kazi kwenye hiyo sinema, hiyo kampuni ya Donna Belajac! Duh!
Kwa habari zaidi za mkasa huo someni: