Arusha ni mojawapo ya miji mizuri ya Tanzania,ni mji uliopo Kaskazini mwa Tanzania.Uzuri wa mji huu ni jinsi ulivyozungukwa na vivutio vingi vilivyopo pembezoni mwa mji huu,mlima mrefu wa Kilimanjaro uko Arusha,Mbuga za wanyama kama Ngorongoro,Tarangire,Mbuga ya Ziwa Manyara na nyingine nyingi zimeuzunguka mji huu wa Arusha. Hali ya hewa ya mji huu wa Arusha ni ya ubaridi kwa karibu kipindi chote cha mwaka hali ambayo huwavutia watu wengi kuutembelea.Ufikapo Arusha utahitaji mahali pa kufikia amabapo ni pa zuri na salama,ni katikati ya mji huu ambapo inapatikana hoteli ya Kibo (Kibo Palace Hotel),ufikapo hapo utajihisi kweli uko Tanzania nchi iliotukuka kwa uzuri na vivutio vya kila aina,angalia mandhari ya Hoteli hii na hutajutia kuwa ndani ya Tanzania na kuwa mtanzania.
Kibo Palace Hotel-Arusha
Kibo Palace Hotel-Arusha
No comments:
Post a Comment