Hili ni toleo lililohifadhiwa la Sheria na Masharti yetu. Tazama toleo la sasa au matoleo yote ya awali.

Sheria na Masharti ya Google

Ilibadilishwa mwisho tarehe: 11 Novemba 2013 (angalia matoleo yaliyohifadhiwa)

Karibu Google!

Asante kwa kutumia bidhaa na huduma zetu (“Huduma”). Huduma zenyewe zinatolewa na Google Inc. (“Google”), kampuni inayopatikana 1600 Amphitheatre Parkway, Mountain View, CA 94043, United States.

Kwa kutumia Huduma zetu, unakubaliana na masharti haya. Tafadhali yasome kwa makini.

Huduma zetu zinatofautiana, kwa hivyo wakati mwingine masharti ya ziada au matakwa ya bidhaa (pamoja na masharti ya umri) yanaweza kutumika. Masharti ya ziada yatapatikana kwenye Huduma husika, na masharti hayo ya ziada huwa sehemu ya mkataba kati yako nasi kama unatumia Huduma hizo.

Kutumia Huduma zetu

Lazima ufuate sera zozote zinazotolewa kwako kwenye Huduma zetu.

Usitumie Huduma zetu vibaya. Kwa mfano, usivuruge Huduma zetu au kujaribu kuzifikia kwa kutumia mbinu nyingine isipokuwa kiolesura na maagizo tunayotoa. Unaweza kutumia Huduma zetu kama inavyoruhusiwa kisheria tu, zikiwemo sheria na kanuni husika za kudhibiti uuzaji na uuzaji tena wa bidhaa kwa nchi za kigeni. Tunaweza kusimamisha au kusitisha utoaji wa Huduma zetu kwako kama hutafuata masharti au sera zetu au kama tunachunguza mwenendo mbaya tunaoshuku.

Kutumia Huduma zetu hakukupi umiliki wa hakimiliki zozote katika Huduma zetu au maudhui unayoyapata. Huwezi kutumia maudhui kutoka kwenye Huduma zetu bila ruhusa ya mmiliki wake au umeruhusiwa vinginevyo kisheria kufanya hivyo. Masharti haya hayakupi haki ya kutumia rajamu au nembo zozote zinazotumiwa katika Huduma zetu. Usiondoe, usifute wala usibadilishe taarifa zozote za kisheria zinazoonyeshwa ndani ya au pamoja na Huduma zetu.

Huduma zetu huonyesha maudhui mengine ambayo si ya Google. Maudhui hayo ni wajibu wa yule anayeyatoa peke yake. Tunaweza kutathmini maudhui ili kuamua kama ni kinyume cha sheria au yanakiuka sera zetu, na tunaweza kuondoa au kukataa kuyaonyesha maudhui tunayoamini yanakiuka sera zetu au sheria. Lakini hiyo haimaanishi ya kwamba tunatathmini maudhui kila wakati, kwa hivyo tafadhali usidhani kuwa tunafanya hivyo.

Kuhusiana na matumizi yako ya Huduma, tunaweza kukutumia matangazo ya arafi za huduma, ujumbe wa usimamizi na maelezo mengine. Unaweza kuamua kujiondoa kwenye baadhi ya mawasiliano hayo.

Baadhi ya Huduma zetu zinapatikana kwenye vifaa vya mkononi. Usitumie Huduma kama hizo katika njia ambayo inakutatiza na kukuzuia kutii sheria za trafiki au za usalama.

Akaunti yako ya Google

Huenda ukahitaji Akaunti ya Google kutumia baadhi ya Huduma zetu. Unaweza kubuni Akaunti yako ya Google mwenyewe, au unaweza kupewa Akaunti ya Google na msimamizi, kama vile mwajiri wako au taasisi ya elimu. Kama unatumia Akaunti ya Google uliyopewa na msimamizi, masharti tofauti au ya ziada yanaweza kutumika na msimamizi wako anaweza kufikia au kufunga akaunti yako.

Ili kulinda Akaunti yako ya Google, weka nenosiri lako siri. Unawajibika kwa shughuli ambayo inafanyika au kupitia Akaunti yako ya Google. Jaribu kutotumia tena nenosiri lako la Akaunti ya Google kwenye programu zingine. Ukitambua matumizi yoyote ambayo hayajaidhinishwa ya nenosiri lako au Akaunti ya Google fuata maagizo haya.

Ulinzi wa Faragha na Hakimiliki

Sera za faraghaza Google huelezea tunavyoshughulikia data yako ya kibinafsi na kulinda faragha yako unapotumia Huduma zetu. Kwa kutumia Huduma zetu, unakubali kwamba Google inaweza kutumia data hiyo kulingana na sera zetu za faragha.

Huwa tunajibu taarifa za madai ya ukiukaji wa hakimiliki na kufunga akaunti za wakiukaji sugu kulingana na utaratibu uliowekwa katika sheria ya U.S. Digital Millennium Copyright Act.

Tunatoa habari kusaidia wenye hakimilki wadhibiti haki zao za uvumbuzi mtandaoni. Kama unafikiria kuna mtu anayekiuka hakimiliki zako na unataka kutujulisha, unaweza kupata maelezo kuhusu jinsi ya kuwasilisha taarifa na sera ya Google kuhusu kujibu ilani kwenye Kituo chetu cha Msaada.

Maudhui yako katika Huduma zetu

Baadhi ya Huduma zetu zinakuruhusu kuwasilisha maudhui. Unabaki na umiliki wa hakimilki zozote ulizo nazo katika maudhui hayo. Kwa ufupi, chako kinabakia ni chako.

Unapopakia au kuwasilisha maudhui vinginevyo kwa Huduma zetu, unaipa Google (na wale tunaofanya kazi nao) leseni ya kutumia, kupangisha, kuhifadhi, kunakili, kurekebisha, kubuni maudhui kutokana nayo (kama yale yanayotokana na kutafsiri, utohozi au mabadiliko mengine tunayofanya ili maudhui yako yafanye kazi vizuri na Huduma zetu), kuwasilisha, kuchapisha, kucheza hadharani, kuonyesha hadharani na kusambaza maudhui hayo, duniani kote. Haki unazotupa katika leseni hii zitakuwa tu kwa ajili ya kuendesha, kukuza na kuboresha Huduma zetu, na kubuni zingine mpya. Leseni hii itaendelea kutumika hata kama utawacha kutumia Huduma zetu (kwa mfano, kwa orodha ya biashara ambayo umeiongeza kwenye Google Maps). Baadhi ya Huduma zinaweza kukupa njia za kufikia na kuondoa maudhui ambayo yametolewa kwa Huduma hiyo. Pia, katika baadhi ya Huduma zetu, kuna masharti au mipangilio inayoweka kizuizi kwa kiwango tunachoweza kutumia maudhui yaliyowasilishwa katika Huduma hizo. Hakikisha kuwa una haki zinazohitajika kutupa leseni hii kwa maudhui yoyote unayowasilisha kwenye Huduma zetu.

Ikiwa una Akaunti ya Google, tunaweza kuonyesha jina lako la Wasifu, picha ya Wasifu, na vitendo unavyovichukua kwenye Google au kwenye programu zingine zilizounganishwa kwenye Akaunti yako ya Google (kama vile +1, ukaguzi unaouandika na maoni unayoyachapisha) katika Huduma zetu, ikiwa ni pamoja na kuonyesha katika matangazo na miktadha mingine ya kibiashara. Tutaheshimu chaguo utakazozifanya ili kuzuia kushiriki au mipangilio ya mwonekano katika Akaunti yako ya Google. Kwa mfano, unaweza kuchagua mipangilio yako ili jina na picha yako zisionekane katika tangazo.

Unaweza kupata maelezo zaidi kuhusu jinsi Google inavyotumia na kuhifadhi maudhui katika sera ya faragha au masharti ya ziada ya Huduma mahususi. Ukitoa maoni au mapendekezo kuhusu Huduma zetu, tunaweza kutumia maoni na mapendekezo yako bila kuwajibika kwako.

Kuhusu Programu katika Huduma zetu

Wakati Huduma inahitaji au inajumuisha programu inayoweza kupakuliwa, programu hii inaweza kujisasisha kiotomatiki kwenye kifaa chako mara toleo jipya au kipengee kipya kinapopatikana. Baadhi ya Huduma zinaweza kukuruhusu urekebishe mipangilio yako ya kujisasisha.

Google inakupa leseni ya kibinafsi, duniani kote, bila ada, isiyoweza kuhamishwa kwa mwingine na isiyowaondoa wengine, ya kutumia programu iliyotolewa kwako na Google kama sehemu ya Huduma. Leseni hii lengo lake la pekee ni kukuwezesha kutumia na kufurahia faida ya Huduma kama zinavyotolewa na Google, kwa jinsi inayoruhusiwa na masharti haya. Huruhusiwi kunakili, kubadilisha, kusambaza, kuuza au kukodisha sehemu yoyote ya Huduma zetu au programu zilizojumuishwa, wala huruhusiwi kufanya uhandisi wa kinyume au kujaribu kudondoa msimbo asili wa programu hiyo, isipokuwa sheria iwe inazuia vikwazo hivyo au una ruhusa yetu kimaandishi.

Programu huria ni muhimu kwetu. Baadhi ya programu zinazotumika katika Huduma zetu zinaweza kutolewa chini ya leseni ya programu huria ambayo tutatoa kwako. Kunaweza kuwa na vipengele katika leseni ya programu huria ambavyo vinabatilisha baadhi ya masharti haya.

Kubadilisha na Kukatisha Huduma zetu.

Tunabadilisha na kuboresha Huduma zetu kila wakati. Tunaweza kuongeza au kuondoa utendakazi au vipengee, na tunaweza kusimamisha au kusitisha Huduma kabisa.

Unaweza kuacha kutumia Huduma zetu wakati wowote, ingawa tutasikitika kukupoteza. Google inaweza kuacha kukupa Huduma, inaweza pia kuongeza au kuweka mipaka mipya kwa huduma zetu wakati wowote.

Tunaamini kuwa unamiliki data yako na kuhifadhi ufikiaji wako kwa data hiyo ni muhimu. Tukiondoa Huduma, inapowezekana, tutakupa ilani ya muda ufaao na nafasi ya kuondoa maelezo kwenye Huduma hiyo.

Hakikisho na Kanusho Zetu

Tunatoa Huduma zetu kwa kutumia kiwango cha ujuzi na uangalifu wa kibiashara unaofaa na tunatumaini utafurahia kuzitumia. Lakini kuna mambo fulani ambayo hatuahidi kuhusu Huduma zetu.

Isipokuwa vile ilivyodhihirishwa katika masharti haya au masharti ya ziada, Google, waletaji au wasambazaji wake hawatoi ahadi yoyote mahususi kuhusu huduma. kwa mfano, hatuweki ahadi zozote kuhusu maudhui ndani ya huduma, kazi mahususi ya huduma, au uthabiti wao, upatikanaji, au uwezo wa kukutimizia mahitaji yako. Tunatoa huduma “kama ilivyo”

Baadhi ya haki za kisheria, zilitoa dhamana fulani, kama dhamana ya kuwa katika hali nzuri ya biashara, ufao wake kwa kazi fulani na isiyokiukwa. Tunatoa dhamana zote ila tu kwa kiasi hicho kilichoruhusiwa na sheria.

Dhima ya Huduma zetu

Wakati imeruhusiwa kisheria, google, na waletaji na wasambazaji wake, hawatawajibika kwa upotezaji wa faida, mapato, au data, fedha kupotea; au uharibifu usio wa moja kwa moja,maalum, wa tukio,wa kipekee, au wa adhabu.

Mpaka kwa kiwango kinachokubaliwa kisheria, jumla ya dhima ya google, na waletaji na wasambazaji wake, kwa madai yoyote chini ya masharti haya, pamoja na dhamana zilizodokezwa, haitazidi kiwango ulichotulipa ili kutumia huduma (au, tukichagua, kukupatia huduma tena).

Katika kesi zote, Google na waletaji wake na wasambazaji, hawatawajibika kwa uharibifu au hasara ambayo haiwezi kutarajiwa.

Tunatambua kwamba kwenye nchi zingine, unaweza kuwa na haki za kisheria kama mlaji. Kama unatumia huduma kwa manufaa yako pekee, basi hakuna cho chote kwenye masharti haya au masharti yo yote ya ziada ynamwekea kiwango mlaji ye yote haki za kisheria ambazo haziwezi kuondolewa na kandarasi.

Matumizi ya kibiashara ya Huduma zetu

Kama unatumia Huduma zetu kwa niaba ya biashara, biashara hiyo inayakubali masharti haya. Itaichukulia Google kuwa bila hatia na itaifidia pamoja na washirika wake, maafisa, mawakala, na wafanyakazi kutokana na madai yoyote, mashtaka au kesi kutokana na au kuhusiana na matumizi ya Huduma au ukiukaji wa masharti haya, ikiwa ni pamoja na dhima au gharama yoyote kutokana na madai, hasara, uharibifu, mashtaka, hukumu, gharama za mashtaka na ada za wakili.

Kuhusu Masharti haya

Tunaweza kubadilisha masharti haya au masharti ya ziada yanayotumika kwa Huduma, kwa mfano, kuonyesha mabadiliko katika sheria au mabadiliko katika huduma zetu. Inafaa uangalie masharti haya mara kwa mara. Tutaweka taarifa za marekebisho ya masharti haya kwenye ukurasa huu. Tutaweka taarifa ya masharti ya ziada yaliyorekebishwa katika Huduma husika. Mabadiliko hayatatekelezwa kwa wakati uliopita na yataanza kufanya kazi baada ya angalau siku kumi na nne baada ya kuchapishwa. Lakini, mabadiliko yanayoshughulikia utendakazi mpya wa Huduma au mabadiliko yaliyofanywa kwa sababu za kisheria yatatumika mara moja. Kama hukubaliani na masharti yaliyobadilishwa ya Huduma fulani, unfaa uache kutumia Huduma hiyo.

Kama kuna ukinzani kati ya masharti haya na masharti ya ziada, masharti ya ziada yatadhibiti ukinzani huo.

Masharti haya yadhibiti uhusiano kati yako na Google. Hayaleti haki zozote kufaidi mhusika mwingine.

Kama hutii masharti haya, na hatuchukui hatua mara moja, hii haimaanishi ya kwamba tunasalimisha haki zozote ambazo tunazo (kama vile kuchukua hatua baadaye).

Ikitokea kwamba sharti fulani haliwezikutekelezwa, hili halitaathiri masharti mengine yoyote.

Mahakama kwenye nchi zingine hazitatumia sheria za California kwa aina zingine za makesi. Kama wewe ni mwenyeji wa mojawapo ya nchi hizo, basi pale sheria ya California haiwezi kutumiwa, sheria za nchi yako zitatumika kwa makesi yale ambayo yanahusiana na masharti haya Amasivyo, unakubali kwamba sheria za California, U.S.A, isipokuwa uchaguzi wa sheria wa California umeamua, zitatumika kwa kesi lo lote linalotokana na au linalohusiana na masharti haya au Huduma zenyewe. Hali kadhalika kama mahakama nchini mwako hazitakuruhusu ukubali mamlaka na mahali pa kufanyia kesi kuwa Santa Clara County, California, U.S.A., mamlaka yenu ya ndani na mahali pa kesi vitatumika kwa makesi yanayohusiana na masharti haya. Amasivyo, madai yote yatokanayo na au kuhusiana na masharti haya au huduma yatashitakiwa tu kwenye mahakama za muungano au za jimbo la Santa Clara County, California, U.S.A., na wewe na Google mnakubali mamlaka ya kibinafsi kwenye mahakama hizo.

Kwa maelezo kuhusu jinsi ya kuwasiliana na Google, tafadhali tembelea ukurasa wetu wa mawasiliano.

Programu za Google
Menyu kuu