Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii
CHUO cha Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi cha Dodoma kimesema kuwa kinatekeleza kauli ya Rais Dk. John Pombe Magufuli katika kuelekea uchumi viwanda katika uzalishaji wa vijana wenye ujuzi wa kutumikia viwanda hivyo.

Hayo yamesemwa leo mkoani Dodoma na Mkuu wa Chuo hicho, Ramadhan Mataka ambaye yupo katika ziara ya kuangalia nafasi ya VETA katika uzalishaji wa vijana katika soko la ajira na fursa ambazo zinazopatikana kuelekea Tanzania ya viwanda.

Amefafanua  kozi zinazozalishwa katika chuo hicho zinamfanya mhutimu kuingia katika soko la ajira bila kuwa na changamoto yeyote kutokana na ujuzi wa walioupata katika chuo hicho.

Ameongeza kozi ambazo zina fursa ya ajira za uhakika  lakini mwitikio wake mdogo ni kozi uchoraji ramani, ujenzi wa barabara na ukarabati ambazo kozi hizo wanafunzi wanaweza kutumika sehemu
kubwa wakala wa barabara wa vijijini na Mjini (Tarula).

Amesema vijana waliotoka kozi hizo wamajiliwa na kampuni za ukandarasi ambapo wamekuwa wakifanya vizuri lakini idadi ya vijana wanaojiunga ikilinganishwa mahitaji yaliyopo katika ujenzi wa barabara na ukarabati pamoja na uchaoraji ramani za majengo.

Mataka amesema katika kuipa uzito kozi ya ujenzi wa barabara na ukarabati wameanzisha lugha ya kichina ambapo wanaasoma kozi hiyo watapohitimu wanaweza kuajiriwa na kampuni za ujenzi za kichina zilizopo nchini kutokana na kujua lugha ya mawasiliano.

Aidha amesema wameanzisha kozi adimu ya watumishi wa kazi za ndani ambapo wakisoma watajua majukumu yao nini wakati wanaingia mkataba kwa kazi wanayoifanya.

Hata hivyo amesema katika kozi mpya ni pamoja utayarishaji na mikato ya Nyama ambapo wanaweza  kutumika katika masoko ya nyama kutokana na mafunzo walioyapata.

Mmoja wa Mwanafunzi wa Kozi ya Ujenzi wa Barababara na Ukarabati, Esther Ipini amesema wasichana wajitoe katika kusoma kozi hiyo kutokana na uhakika wa ajira na kuongeza hakuna kazi ambazo ziko kwa ajili ya wanaume kwani huko ndiko kunafanya wanawake kuwa nyuma kimaendeleo sasa ni wakati wa kujitoa kila sehemu tukapata ujuzi.
 Mkuu wa Chuo cha VETA, Dodoma, Ramadhan Mataka akizungumza na waandishi habari kuhusiana maendeleo ya chuo hicho katika kuzalisha vijana wa kuweza kutumika katika sekta ya viwanda, jijini Dodoma.
 Meneja wa Mawasiliano wa VETA, Sitta Peter akizungumza na waandishi habari kuhusiana na umuhimu wa waandishi kuandika fursa za vyuo vya VETA , jijini Dodoma.
 Mwanafunzi wa mwaka wa tatu wa kozi ya Ujenzi wa Barabara na  Ukarabati wa Barabara, Khadija Mohamed akizungumza na waandishi habari kuhusiana na umahiri anaoupata katika kozi hizo, jijini Dodoma.
 Mwanafunzi wa kozi ya utayarishaji na mikato ya Nyama Victoria Massawe akizungumza na waandishi habari namna  ya kuandaa nyama kuanzia uchinjaji mpaka kumfikia mlaji leo jijini Dar es Salaam.
 Wanafunzi wa kozi ya Ujenzi na Ukarabati wa Barabara wakionesha waandishi kuhusiana mafunzo wanayopata katika kozi hiyo.
Wanafunzi wa ukatibu muhtasi wakiwa darasani na mashine za kuchapa

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...